Kupitia Insta Story yake Msanii Harmonize (Rajab Kahali) chini ya Menejimenti ya Konde Music Worldwide ameiomba radhi Serikali kwa kosa la kupakia mtandaoni wimbo wake alioutoa hivi karibuni ufahamikao kama “WEED LANGUAGE” ambao ulikuwa umesheheni maudhui ya Bangi kwa vile umekuwa ukitaja majina tofauti ya bangi inavyoitwa katika maeneo mengine hapa duniani.
Serikali haikuwa kimya, kupitia Wizara yenye dhamana ya kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini ilitoa tamko kali kuhusu kupinga na kuchukua hatua kwa yeyote atayejihusisha na kuachia wimbo unaohamasisha matumizi ya madawa ya kulevya hasahasa zaidi matumizi ya bangi, Sheria itafuata mkondo wake juu ya kitendo kama hicho.
Msanii huyo ameamua kutii amri kwa kuahidi kuufutilia mbali wimbo huo uliopo kwenye majukwaa tofauti ya mtandaoni.