Kamati ya Tuzo za TFF imempitisha Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele kuwa Mshindi wa tuzo ya Mchezaji bora wa mwezi Novemba wa Ligi Kuu soka Tanzania bara 2022/2023 kwa kufunga magoli 7 ambapo Mayele alikuwa akiwania tuzo hiyo na Moses Phiri wa Simba SC na Saido Ntibazonkiza wa Geita.
Baada ya kikao cha kamati ya tuzo za TFF kilichokutana jijini Dar es salaam siku ya Jumanne December 6 2022 kilimchagua Mayele kutokana na kuonesha kiwango kizuri kwa mwezi Novemba na kutoa mchango mkubwa ndani ya kikosi cha Yanga SC.
Zaidi ya hilo katmati hio kupitia kikao hicho kilimchagua Kocha mkuu wa Simba SC Juma Mgunda kuwa ndiye kocha bora wa mwezi Novemba.