
Benki ya NBC kupitia Kampeni yake ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar imeeleza kuwa… “Safari Imeiva! Washindi wa wanne wa Kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar inayoendeshwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wamewasiri jijini Dar es Salaam kutoka mikoa mbalimbali tayari kwa ajili ya kuanza safari hii leo kuelekea nchini Qatar kushuhudia mechi ya Robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 kati ya Uingereza na Ufaransa itayochezwa Disemba 10, mwaka huu.
Washindi hao kutoka mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Singida na Dar es Salaam jana walipokelewa rasmi jijini Dar es Salaam na Benki ya NBC na kutambulishwa rasmi katika hafla fupi ya jioni iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wa mchezo wa soka nchini sambamba na maofisa wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa wateja Wadogo wa NBC, Bw. Elibariki Masuke”.