Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amewataka wafugaji kubadili mbinu ya ufugaji kutoka ule wa asili ambao umekuwa kichocheo cha migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji.
kubadilika kwa Wakulima hao kwa kutumia mbinu mbadala za ufugaji italeta tija kwa kuwa na Mifugo michache katika eneo moja lakini kupata kipato kikubwa ambacho kitaendelea kukuzi mahitaji ya kila siku pia, kuondoa kabisa migogoro ya ardhi inayojitokeza kila pachao katika baadhi ya maeneo ya hapa nchini.