Mshambuliaji wa Yanga SC mwenye Jezi namabri 49, Clemeny Mzize azidi kuwa tishio kwa timu pinzani kutokana na ubora wake kuweza kuongezeka maradufu ya hapo awali.
Mshambuliaji huyo ameonesha uwezo mkubwa kwa kufunga Goli 3 (Hattrick) katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho la AZAM SPORTS dhidi ya Kurugenzi FC ambapo kwa jumla ilipata ushindi wa magoli 8-0.
Aidha Clement alipata kuaminiwa na Kocha Mkuu Nabi na kupewa nafasi ya kujiunga na Kikosi cha Kwanza Kinachoshiriki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara akitokea Timu (kikosi) B, bado ameweza kuonesha makali yaleyale aliyokuwa nayo kipindi yupo Yanga B.
Ubora anaoudhihirisha akicheza Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho unawafanya mashabiki wa klabu hio kuwa na furaha zaidi na kuvutiwa kumtazama mshambuliaji huyo akiwa angali kijana mdogo akipeleka mashambulizi kwa timu pinzania katika mechi husika.