
WAZIRI mwenye dhamana ya Tamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Mohamed Mchengerwa amegusia swala zima la kuwiwa sana Nchi ya Tanzania Kushiriki Michuano ya Fainali za Kombe la Dunia chini ya FIFA.
Waziri Mchengerwa amefunguka kuhusiana na hilo kupitia kituo cha kurusha matangazo cha Clouds Media, kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam.
“Tunataka twende tukashiriki kombe la Dunia 2030 na kila jambo linawezekana na tumepata bahati Rais wetu wa CAF anataka Bara la Afrika ziende timu 9 (kwa sasa timu 5) hatuna sababu kwanini tukose kwenda kwenye Fainali za kombe la Dunia 2030.” Mohamed Mchengerwa
“Wizara ya Michezo inaleta utulivu kwa Watanzania pale ambapo unaona unakereka kidogo basi unakwenda kuangalia Simba na Yanga. Wizara ina watu wenye ushawishi na inafuatiliwa na Watanzania wengi kwa sababu zile sekta zilizopo kwenye wizara hii zinawagusa Watanzania moja kwa moja”