
Rais Dkt.@SuluhuSamia amepewa tuzo ya International Iconic Awards ya nchini India kwa kutambua mchango wake katika kuasisi na kushiriki kwa umahiri mkubwa katika programu ya Tanzania – The Royal Tour ambayo imekua na matokeo chanya kwa jamii inayomzunguka.
Tuzo hiyo imekabidhiwa jijini Dodoma na uongozi wa Miss Jungle International na Bega kwa Bega na Mama (BBMF) kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana.


