Taifa la Peru linadhihirisha ugumu zaidi katika kuliongoza kwani kwa miaka minne pekee tayari imeweza kuongozwa na jumla ya Marais 6.
Pedro Castillo alikuwa rais wa mwisho kuondolewa, lakini yeye na watangulizi wake wanagawana muda mfupi waliohudumu madarakani
Mrithi wake, Dina Boluarte aliyeapishwa hivi karibuni, anakuwa rais wa kwanza mwanamke katika historia ya Peru, lakini pia kiongozi wa sita wa taifa hilo la Peru tangu 2018 (Pedro Pablo Kuczynski, Martín Vizcarra, Manuel Merino, Francisco Sagasti, Pedro Castillo na Dina Boluarte )
Hali hiyo inakuwa tishio kutokana na watu wengi wa Peru wamezoea kuishi nje ya siasa na misukosuko yake ya kudumu.