
Katika kuenzi maadhimisho ya miaka 58 ya siku ya Jamhuri ya Kenya, Vodacom ilipata nafasi ya kushiriki kwenye ‘Kenya Diaspora Forum’ hafla iliyoandaliwa na ubalozi wa Kenya nchini Tanzania mahsusi kwa wana Diaspora wa Kenya waliopo Tanzania. Pamoja na mambo mengine, wana Diaspora walipata nafasi ya kujifunza kuhusu fursa za kiuchumi na kijamii zinazoletwa na huduma za kampuni hio ya mawasiliano nchini, za kibunifu hasa Kutuma Pesa kimataifa (IMT) pamoja na huduma ya 5G ambayo ni ya kwanza na pekee nchini Tanzania.