
Kituo cha Afya Hombolo kilichopo katika Jiji la Dodoma kimeanza kutoa huduma za mionzi kwa wananchi wa kata hiyo na maeneo ya jirani mara baada ya kupokea mashine ya X-ray kutoka Serikali kuu.
Akizungumza baada kupokea Mashine hiyo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Dkt.Andrew Method amesema hapo awali wananchi wa hombolo walilazimika kuja mpaka vituo vya mjini ambapo ni mbali na makazi yao mara tu wanapohitaji huduma hiyo.
“Lakini kwa sasa huduma hiyo imesogezwa karibu kabisa na wananchi hao hivyo itakua imewapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya mionzi, Dkt. Andrew.
Mashine hiyo ya X-ray ni miongoni mwa mashine 137 zilizopelekwa kwenye vituo vya kutolea huduma nchini kote.
Tunamskuru Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kusogeza huduma za Afya karibu kabisa na wananchi.

