Mshambuliaji wa Kikosi cha Simba Queens na Timu ya Taifa ya Wanawake, Opah Clement aanza kwa kuwa kinara wa kufunga magoli zaidi katika Ligi ya Mpira wa Miguu kwa Upande wa Wanawake nchini inayodhaminiwa na SERENGETI LITE.
Nyota huyo amekuwa na mwanzo mzuri wa msimu kupitia mechi za awali alizocheza katika mzunguko wa msimu wa mwaka 2022/2023, japo bado Timu yake ikishikilia nafasi ya nne wakati Mabingwa wa zamani JKT Queens wapo kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite.