Baada ya kukamilisha taratibu za Sajili za Nyota wa soka wa Ureno na kufanya Utambulisho wake mnamo klabu husika ya Al-Nassr FC sasa utaratibu mwingine wa ziada kwa mchezaji huyo umefanyika.
Klabu ya Al-Nassr FC imemuandalia nyota wake mpya Cristiano Ronaldo hoteli ya kifahari yenye hadhi ya nyota tano iliyopo mji wa Riyadh makao makuu ya nchini Saudi Arabia ili nyota huyo aishi na familia, marafiki na walinzi wake hadi mkataba wake utakapomalizika.