Mwenyekiti wa kamati ya sheria na hadhi za Wachezaji, TFF Ndug. Said Soud amesema Wachezaji wengi huwa wanasaini mkataba baada ya kusoma ukurasa unaoonesha mshahara watakaolipwa pekee lakini hawapitii karatasi nyingine zenye vifungu vyenye masharti ya utekelezaji wa Mkataba husika”
“Feisal alisimamia kifungu kimoja wakati mkataba huundwa kwa vipengele vingi, ambapo unapaswa uvisome vyote kwa pamoja”
“Hata hivyo sisi tunasikia kama wewe ulivyosema kuwa Azam inahusika katika kumshawishi Feisal ambapo kimsingi ni kosa. Ikibainika kuwa Azam FC wamemshawishi Feisal kuvunja mkataba na Yanga bila kufuata utaratibu, Azam tutaifungia na hata Feisal atafungiwa kushiriki Soka la Mpira wa Miguu-Said Soud