Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro zimesababisha madhara mbalimbali kwa wakazi wa mkoa huo ikiwa ni pamoja na, mafuriko, kubomoka kwa baadhi ya Nyumba na foleni ya magari Barabara kuu ya Morogoro kwenda Dodoma.
Kukirhiri kwa mvua hio kumemfanya Mbunge wa Jimbo la Manispaa Morogoro Mjini Ndugu Abdul-aziz Abood kujitoa kuungana na jamii yake ya jimbo hilo ili kupata wazo la kunusuru baadhi ya kaya zilizzopata Dhoruba ya Mafuriko ya Maji yaliopelekea kupbomoka kwa sehemu zao za makazi hii leo Ijumaa ya Januari 13,2022.