Afisa Mkuu wa Teknolojia na Mabadiliko ya Kidijitali Benki ya NMB – Kwame Makundi alimkabidhi mshindi wa kwanza katika michuano ya kombe la Mapinduzi Timu ya Mlandenge FC kutoka Zanzibar hundi ya sh. Mil 30 kama sehemu ya udhamini wake katika michuano hiyo.
Benki hio ikiwa inaunga mkono michuano ya Mapinduzi (Mapinduzi Cup), baada ya mechi ya finali iliyochezwa januari 13,2023 kati ya Mlandege na Singida Big Stars mbele ya Rais wa Zanzibar – Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ashuhudia tukio zima la kukabidhi hundi hio.
Zaidi ya hilo benki imezipongeza timu zote zilizoshiriki na kuendeleza ushirikiano na serikali ili kusaidia kukuza michezo nchini.