Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), ambao ni wasimamizi wa mradi huo imetangaza nauli mpya zitakazoanza kutumika Leo Januari 16, 2023.
DART…..”Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) unapenda kuwaarifu watumiaji wa Mabasi Yaendayo Haraka, kuwa kuanzia Jumatatu, Januari 16, 2023 nauli mpya zilizoidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) zitaanza kutumika”

Zaidi ya hilo imetoa ushauri kwa watumiaji wa huduma hio kwamba ili kuepuka kupanga foleni ya kukata tiketi isiyo ya lazima, wapakue sasa App ya Dar City Navigator, ili akate tiketi yake ya safari mahala popote pale alipo.