
Akizungumza Mganga mkuu wa Wilaya ya Itilima Dkt. Anold Musiba amesema “Tumefanimiwa kuanza kutoa huduma ya upasuaji kwa kina Mama wajawazito wanoshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida kutokana na sababu mbali mbali pia tumeanzisha huduma ya watoto njiti pamoja na wale wanaohitaji uangalizi wa karibu sana baada ya kuzaliwa(NICU)”.
Pia Dkt. Anold Musiba ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwanamna inavyojitoa kuhakikisha huduma bora za afya zinawafikia watanzania wote kokote kule waliko.
