Klabu ya Yanga imefanya mpango wa kumrejesha kwa mkopo moja ya aliyewahi kuwa golikipa wake hapo awali, Metacha Manata kutokea klabu ya Singida Big Stars.
Hakika kulingana na Ubora anaouonesha kipa huyo pindi akiwa uwanjani, umewavutia tena Wanayanga kumrejesha kikosini.
Kupitia sajili za dirisha dogo ambalo limefungwa mnamo Januari 15, 2023 Klabu hio imefanikisha zoezi zima la kukamilisha usajili wa mlinda lango huyo na kutambulisha rasmi hapo jana.