Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh. Jokate Mwegelo atarajia mazuri zaidi juu kukamilika kwa haraka kwa miradi ya ujenzi wa njia za uchukuzi nchini hususani miradi iliyopo chini ya Usimamizi wake katika wilaya hiyo ambayo itasaidia watumiaji wa barabara hizo kuondokewa na kero ya foleni zisizokuwa na tija.
DC Jokate @jokateM amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akisema….. “Ndugu zangu wa Mbagala; Nzasa-Kilungule mpaka Buza tujuane tafadhali, Hatua ya Mkeka wenu unaokwenda kupunguza foleni ya Kilwa Road. Wenzangu wa Mbande- Chamazi short cut ya kwenda mjini!! Daraja linakamilika namna hiyo”.
Miradi hio ya barabara imepewa kipaumbele ili kutekeleza ilami ya Serikali iliyopo madarakani katika kuhakikisha inakamilika kwa wakati ili shughuli za kijamii zifanyike bila kikwazo kwa kipindi inapogusia sekta ya Uchukuzi.