
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huu alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
– Mhe. Dkt. Philip Mpango ambapo alielezwa na Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi – Ferdinand Mpona namna benki hio ilivyoshiriki kwenye uzinduzi huo na mchango wa benki pia kwa ujumla katika kufanikisha miradi ya maendeleo nchini.
