Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania Nasibu Abdul (Diamond Platnumz) amekiri kuhamishia mapenzi yake ya ushabiki wa Mchezo wa miguu kwa Klabu ya Yanga akiacha kushabikia klabu yake pendwa ya zamani Simba SC.
Ameeleza hayo kwa kulenga kuwa alishawishika kushabikia klabu ya Simba kutokana na Ushawishi wa Haji Manara na hivyo kuchukua hatua ya Kushabikia Yanga SC imempendeza kwasabau amesema “ALIPO HAJI MANARA NA YEYE YUPO”.