Mfanyabisahara na msanii wa mziki wa kizazi kipya Zena Yusuf Mohammed alimaarufu kama Shilole “Shishi Baby” ameumizwa sana na maamuzi ya kuvunja sehemu yake muhimu ya Kuuzia chakula ifahamikayo kwa jina la SHISHI FOOD ambayo pia huitegemea kwa ukubwa sana kujiingizia kipato cha kila siku ili kupisha zoezi la kiserikali Manispaa ya Kinondoni.
Msanii huyo ameguswa zaidi na hilo kutokana na jinsi alivyojitoa kwa hali na mali kuweza kuifanya biashara hio ya huduma ya chakula iaminike na kutengeneza jina lake kwa muda zaidi akiongezea kwa kusema anahofia kuwapoteza wateja wake wengi waliozoea kufika katika eneo hilo kupata huduma ya chakula chake.
Uamuzi huo wa kuvunjwa umekuja baada ya kupisha ujenzi wa kituo cha afya.