
Meneja wa habari na Mawasiliano Klabu ya Simba, Ahmed Ally afunguka haya kuhusiana na tukio lililowashtua mashabiki wengi wa Klabu hio katika mchezo wao uliochezwa ndani ya dimba la Mkapa dhidi ya Mbeya City FC.
“Watu wote waliokuwa uwanjani na waliokuwa wanatazama kupitia TV tulishtuka kuona Kocha Robertinho anamtoa Chama!”
“Baada ya kushtuka kuna watu ambao tukaamua kusubiri kuona Kocha anataka kufanya nini halafu wapo waliosema huyu Kocha hatufai! Waliosema huyu Kocha hatufai hadi sasa hivi wameshikilia msimamo huo.”
“Tulioamua kusubiri kuona kocha atafanya nini alitujibu palepale uwanjani, baada ya muda mfupi tukaona kwa nini aliamua kufanya mabadiliko yale.”
“Maamuzi aliyoyafanya ni kwa maslahi ya timu, kwa jicho lake la kiufundi aliona pamoja na ubora wote wa Chama lakini kwenye mchezo ule alihitaji mtu mwingine.”
“Kiutawala sisi tumefurahi kuona tuna mwalimu ambaye anaweza kufanya maamuzi magumu! Kwenye maisha huwezi kufanikiwa kama huwezi kufanya maamuzi magumu.”


