Mwanaume mmoja ambaye hajafahamika jina lake hapo jana Januari 19, alikutwa amepanda kwenye nguzo ya umeme wa msongo wa kilovoti 132 kwenye njia ya Mwanza-Musoma wilayani Bunda mkoani Mara.
Aidha zoezi la kumuokoa lilifanikiwa na alishuka kwenye nyaya hizo jana majira ya saa 1:00 jioni
Mhandisi wa usafirishaji umeme mkoa wa Mwanza na Mara Shakiru Abdallah, amesema kwamba kijana aliyepanda juu ya nguzo ya umeme wa msongo wa kilovoti 132 kwenye njia ya Mwanza- Musoma, anakabiliwa na changamoto za matatizo ya afya ya akili.