Afisa Mtendaji Msaidizi wa Klabu ya Singida Big Stars Muhibu Kanu amethibitisha kutokea kwa kifo cha aliyekuwa mchezaji na kapteni wa timu ya vijana (U17), Mohammed Banda, kilichotokea jana asubuhi Januari 19, 2023.
Mchezaji huyo aripotiwa kuwa alikuwa anakitumikia kikosi hicho cha U17 katika nafasi ya Beki (Defender).
Banda alipoteza maisha alipofikishwa Hospitali ya Mkoa wa Singida baada ya kugongana kichwani na mchezaji mwenzake wakiwa mazoezini katika Uwanja wa Magereza, Singida.