
Zaidi ya hilo Jacinda Ardern ambaye bado anashikilia rekodi ya kuwa mwanasiasa wa kike mdogo zaidi kushikilia wadhifa wa juu wa Serikali Duniani baada ya kuchukua wadhifa huo mnamo 2017 akiwa na umri wa miaka 37, ataendelea kusalia kama mbunge wa kawaida mpaka uchaguzi wa Oktoba.
“Naondoka kwa sababu jukumu la upendeleo kama hili huja kwa kuwajibika. Kuwajibika ni kujua kama wewe ni mtu sahihi kuongoza au sio. Najua kazi hii inachukua nini. Na ninajua kuwa sina tena vya kutosha kwenye tanki kuitendea haki kazi hii. Ni rahisi hivyo,” amesema Jacinda Ardern.