Mwenyekiti wa Simba SC @SimbaSCTanzania ambaye anamaliza muda wake na anaomba kura za kuendelea kugombea nafasi hiyo kwenye uchaguzi unaotarajia kufanyika Januari 29, Murtaza Mangungu amekiri kuwa basi la timu hiyo limeuzwa na sio bovu kana inavyoelezwa.
“Nashushiwa lawama ambazo sio zangu basi la Simba limeuzwa mimi nikiwa sipo kwenye uongozi sikuwa Mjumbe wa Bodi wala Mwenyekiti wa timu hii kama nilivyo sasa,” Murtaza Ally Mangungu Mwenyekiti wa Simba SC anaegombea kurudi madarakani.
“Lakini baada ya kuingia kwenye uongozi hili suala lilipelekwa kwenye Bodi ya klabu na wajumbe tumelifuatilia na kubaini kuwa (Basi) limeuzwa kwa kufuata utaratibu,” Murtaza Ally Mangungu Mwenyekiti wa Simba SC anaegombea kurudi madarakani.