Kupitia Mkutano na Waandishi wa Habari ulioitishwa na Uongozi wa Klabu ya Simba hapo jana na Kufanyika leo hii mapema mida ya 3:30 asubuhi eneo la SERENA HOTELS, Dar es Salaam, kumekuwa na mengi yaliyozungumzwa kuhusu ujio wa klabu ya Al Hilal ya nchini Sudan hapa Tanzania.
Klabu ya Al Hilal ya nchini Sudan kesho inatarajiwa kuja nchini kuweka kambi ya kujiandaa na michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba SC tutakuwa wenyeji wao.
Wakiwa nchini watacheza michezo mitatu ya kirafiki dhidi ya Simba SC, Azam FC na Namungo FC. Mchezo wetu dhidi ya Al Hilal utakuwa wa mwisho na utachezwa Februari 5, 2023 kwenye Uwanja wa Mkapa.


