
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ametoa Elimu kwa wananchi wa kata ya Orkolili Wilaya ya Siha juu ya umuhimu Bima ya afya na namna itasaidia kuepuka gharama za matibabu kutoka ngazi ya Zahanati mpaka hospitali ya Taifa.
Sambamba na hilo amesema, Kata ya Orkolili imepokea kiasi cha shilingi Bilioni 1.3 kwaajili ya kuboresha huduma katika kata hiyo ikiwemo huduma za afya.
Aidha, Amesema Serikali imeongeza Milioni 150 kwaajili ya ununuzi wa vifaa tiba vitavyotumika katika kituo cha afya cha Orkolili ili wananchi waanze kunufaika na huduma katika kituo hicho.

