Klabu ya Simba imeeleza kwamba Kocha Mkuu wa Klabu hiyo Roberto Oliveira (62) ameondoka usiku wa kuamkia leo kwenda nchini kwao Brazil kwa shughuli binafsi za kifamilia na anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa mwezi huu.
Kocha Roberto aondoka Tanzania na kurejea kwao Brazil ikiwa amefikisha siku 21 toka aanze kukinoa kikosi cha klabu hio kama Kocha Mkuu wa klabu hiyo baada ya kutambulishwa rasmi January 03,2023.
Kocha huyo alijizolea umaarufu Afrika Mashariki kutokana na kuwa game plan nzuri kwa Vipers SC ya Uganda ambao ndio waliwatoa TP Mazembe kwenye Club Bingwa Afrika msimu huu.