Takwimu za mshambuliaji mahiri wa Simba Queens Tanzania Opah Clement zinazidi kudhihirisha ubora wa hali ya juu aliokuwa nao mchezaji huyo katika nafasi yake Ligi Kuu ya Wanawake ya Selengeti Lite, Tanzania Bara.
Opa akiwa amekwishacheza jumla ya mechi 6 ndani ya dakika 518 anaibuka kinara wa ufungaji wa jumla ya magoli 8.
Nyota huyo kwasasa anazidi kuweka mizizi ya kuaminika zaidi akicheza kama winga na Mshambuliaji kutokea pembeni.