Ikiwa ni siku chache hapo nyuma klabu ya Everton kuripotiwa kuwa inawezekana kushuka daraja msimu huu kwa sasa taarifa zilizohusiana na hio ni kuwa klabu hio inauzwa.
Everton imewekwa sokoni na inauzwa kwa bei ya pauni milioni 500. (Guardian) Hata hivyo mmiliki Farhad Moshiri amekanusha taarifa za uwezekano wa kuuzwa, akisisitiza kuwa amejitolea kuitumikia klabu hiyo inayokabiliwa na matatizo na hatari ya kushuka daraja. (Liverpool Echo)