Baada ya siku chache kuripotiwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe, Tundu Lissu atarejea rasmi nchini Tanzania ifikapo Januari 25,2023, kwa taarifa za karibuni anaripotiwa tayari amewasili nchini.
Mchana huu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara) Mhe. Tundu Lissu @TunduALissutayari amewasili Uwanja wa Mwalimu Nyerere na kupokelewa na Katibu Mkuu wa Chama Mhe. Mnyika@jjmnyika
. Muda mchache ujao msafara wake utaelekea viwanja vya Bulyaga uliopo Temeke mwisho, ambapo utafanyika mkutano wa hadhara.Makamu M/kiti wa Chama (Bara) Mhe. @TunduALissu akisalimiana na Wajumbe wa Kamati Kuu Mhe.@HecheJohnna Mhe. @MsigwaPeteralipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere. Muda mchache ujao msafara wake utaelekea viwanja vya Bulyaga, ambapo utafanyika mkutano wa hadhara.