Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna akiwasilisha taarifa ya fedha ya mwaka 2022, amewashukuru wateja na wadau wote kwa kuwa sehemu ya mafanikio ya benki hio.
Bi. Ruth ameweka bayana kuwa 2022 umekuwa mwaka ulioweka historia kwa benki hio, na hii ni kupitia ushirikiano mzuri kati benki ya NMB na wadau wake.
Kupata faida baada ya kodi ya shilingi Bilioni 429, ikiwa ni ongezeko la 47% kulinganisha na mwaka 2021.
Kwa mara ya kwanza katika miaka 25 ya historia ya NMB, mapato ya jumla yalivuka shilingi trilioni moja baada ya kufikia shilingi trilioni 1.2, ongezeko la 23%.
Jumla ya mali za benki zilivuka kiasi cha shilingi trilioni 10 na kufikia shilingi trilioni 10.25, ikiwa ni ukuaji wa kasi wa mizania wa 18% kwa mwaka.
Tuliendeleza ajenda ya ujumuishaji kifedha tukiwa na akaunti za benki zaidi ya milioni sita, hii ni idadi kubwa zaidi ya wateja kwa taasisi moja ya fedha nchini.