Kampuni ya Mawasiliano Tigo Tanzania ikiambatana na Mabalozi wake wa Promosheni ya tiGo Wakishua ambao ni Mtangazaji wa Clouds Media Millard Ayo pamoja na Msanii Marioo, imemkabidhi rasmi mshishi wa Droo kubwa ya Promosheni hio Gari aina ya TOYOTA RUSH 0Km.
Promosheni hio imekuwa ya Tatu kutoka kampuni nhio ianze kutoa Michongo yake ili kuhamasisha Wateja wake kutumia TIGOPESA APP na kuwawezesha kupata ushindi wa kipekee utaowafanya waweze jinykulia Zawadi tofauti.
Hapo awali Tigo ilianza na Mchongo wa TIGO wa Kishua kwa Kuapata nafasi ya Kusikiliza Nyimbo kupitia app ya muziki ya BoomPlay pale kila ununuapo salio kwa kutumia Tigopesa, Baada ya hapo ikafuatia TIGO wa Kishua Twenzetu Qatar na Hisense katika msimu wa Kombe la Dunia 2022.