Rais Samia Suluhu ameshiriki maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Sheria na kuweka bayana baadhi ya masuala yahusianayo moja kwa moja na sheria, Zifuatazo ni sehemu ya Nukuu zake katika tuki hilo;
“Natoa wito kwa Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Fedha, pamoja na mwanasheria mkuu na wote wanaohusika kushirikiana na kuzifanyia marekebisho sheria zote zenye mizunguko inayochelewesha kesi na upatikanaji wa haki mapema”
“Ni matarajio yangu ifike wakati watanzania waone kwamba kufikishana mahakamani sio jambo la lazima, ila tu ni pale inapobidi, badala yake usuluhishi iwe ndio njia ya kwanza ya kukimbilia”
“Kuna msemo maarufu kwamba haki hupewi mkononi lazima uitafute, lakini katika kutafuta haki kuna ujuzi, na wananchi wetu wengi hawana ujuzi wa kutafuta haki zao kwahiyo tuwasaidie kutafuta au kupata haki zao”