Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha Nchini SportPesa yaeleza kusikitishwa sana na uamuzi uliyochukuliwa na Uongozi wa Klabu ya Yanga kuingia makubaliano ya Udhamini wa Michuano ya Kombe la Shirikisho CAF na kampuni nyingine pasipo kufikia muafikiano nayo.
Ikiwa ikiwa siku chache klabu ya Yanga imetoka kumtangaza mdhamini mpya kampuni ya HAIER kwa michuano ya CAF ambaye Logo yake imetumika kwa kuiondoa logo ya mdhamini aliyekuwa naye kwa muda mwingi na bado akiwa anasalia na sehemu ya muendelezo wa mkataba nae, imejenga hali ya sintofahamu kubwa kwa mdhamini huyo.
Kulingana na makubaliano baina ya pande mbili, kampuni ya SportPesa na Yanga ilitakiwa kuwekwa neno “Visit Tanzania” kwenye jezi kwa niaba ya SportPesa na sio hivyo ilivyotokea kwa sasa kumtumia mdhamini mwingine.
Kwa mujibu wa sheria na kanuni za udhamini inajidhihirisha kuwa klabu hio haijaenenda sawa kwa kufuata taratibu maalum baina yake na kampuni ya Sportpesa juu ya kuchukua maamuzi ya kusaini kandarasi mpya ya udhamini bila muafikiano wa pande mbili.