
Raia hao wamekamatwa kufuatia Operesheni maalum inayofanywa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na idara ya misitu ambapo tayari mashamba yenye hekari zaidi ya sita yaliyolimwa bangi yameteketezwa.
Akizungumza wakati wa uteketezwaji wa mihadarati hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Bi.Grace Kingalame amesema hayupo tayari kuona baadhi ya watu wakifanya biashara ya kulima bangi wilayani humo na kuwataka wenye tabia hiyo kuacha mara moja.
Watu hao wamekamatwa kufuatia operesheni inayofanywa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo Grace Kingalame kwa kushirikiana na jeshi la polisi pamoja na idara ya misitu ambapo tayari mashamba yenye hekari zaidi ya sita yaliyolimwa bangi yameteketezwa.