
Mshambuliaji wa PSG na Timu ya Taifa ya Brazil, Neymar Jr ameshinda tuzo ya Samba d’or kwa mwaka 2022.
Samba d’or ni tuzo ambayo hutolewa kwa mchezaji bora wa mwaka kutoka Brazil.
Neymar ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya 6 kwenye maisha yake ya soka na ndio mchezaji mwenye idadi kubwa (6) ya tuzo hiyo tangu kuanzishwa kwake mnamo 2008.
Thiago Silva ni Mbrazil anayefuatia kwa kuwa na idadi kubwa Samba d’or ambaye ametwaa mara tatu.
