
Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutokea San Diego kuelekea Newark lakini takribani dakika 45 tangu kuanza kwa safari ndege hiyo ililazimika kurudi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa San Diego.
Wafanyakazi wa Ndege hiyo ndio waliofanikiwa kuidhibiti kompyuta hiyo na kuuzuia moto kusambaa.
Dharura za aina hii ndizo zinazopelekea sheria za usafiri wa anga kutoruhusu vifaa kadhaa vya kielektronika kuwekwa kwenye mizigo inayohifadhiwa chini ya ndege kwani vifaa hivyo huweza kulipuka wakati wowote.