Baada ya mchakato wa kutaka kumaliza sintofahamu inayojitokeza baina ya Dr Mwaka na Mkewe kuhusiana kutokuwa sawa kwa muda na hivyo kuhitaji kutalakiana, Mke wake ghafla ajitokeza katika vyombo vya habari ili kuiomba serikali iweze kuingilia kati suala hilo liweze kupata suluhu ya moja kwa moja.
Mwanamke huyo ameonekana kupitia mtandao akizungumza na waandishi wa habari ili kuweza kufikisha ujumbe kwa Serikali iliyopo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu kuweza kuelekeza jitihada zake katika kutatua jambo hilo kwa haraka ili aweze endelea kuishi kwa amani.
Aidha kwa namna alivyojieleza inaonesha dhahiri anakosa amani hivyo kumsihi Dr Mwaka aseme anachokitaka kinachohusiana na mali ili amuachie anachokitaka na aweze ishi na familia yake kwa amani.