Mkurugenzi wa Makampuni ya METL Group na Mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji MO kupitia ukurasa wa Twitter wa Mzabuni wa Kuzalisha jezi za klabu hio Fred Fabian Ngajiro (Fred VunjaBei) ame comment juu ya kutaka kujua kwanini kwenye jezi mpya zitazoenda tumika katika michuano ya klabu Bingwa Afrika, Matangazo ya MO yametolewa?….
Mashabiki na Wadau wengine wa soka wamechagiza zaidi kwa kuandika jumbe za kumkosoa na kumshauri mzabuni huyo juu ya mwenendo wake katika suala zima lihusianalo na matayalisho ya Jezi.
Hapo wadau wengi waendelea kuwa na shauku kubwa kufahamu nini kitaendelea juu ya swali hilo.