
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson ameshauri Taifa kufahamu utaratibu mzuri wa kutumika linapokuja suala la utoaji wa Degree za heshima kwa kuwa kuna wakati zinatolewa kama pipi na kutolewa kwa kila Mtu, jambo ambalo amesema halikubaliki kwa kuwa linalivunja heshima ya Taifa kwenye eneo la elimu na kwenye kuwapa heshima wanaostahili.
Kauli hiyo ya Spika Dr. Tulia Ackson inakuja baada ya Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi kuomba mwongozo kwa Spika kutaka kufahamu Vyuo vinavyotoa udaktari wa heshima ni kwa kiasi gani vinatambulika katika Mamlaka zinazosimamia elimu nchini pia baadhi ya Wabunge wenye muda mfupi Bungeni kutunikiwa Degree za heshima na Wakongwe kutopata hivyo ametaka kujua ni vigezo gani vinatumika.