
Amesema hayo leo tarehe 09 Februali 2023 Bugeni Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Mhe. Francis Leonard Mtega aliyetaka kujua Je, ni lini Serikali itapeleka Vifaa Tiba katika Hospitali ya mpya ya Wilaya ya Mbarali.
Dkt. Dugange amesema Serikali imepeleka vifaa na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 418 kwa ajili ya jengo la huduma za dharura (EMD), pamoja na mashine ya kisasa ya X-ray ya shilingi milioni 155 hospitali ya Wilaya ya Mbarari katika mwaka wa fedha 2022/23.
Aidha, Dkt. Dugange amesema Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi milioni 100 katika bajeti ya mwaka 2022/23 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwenye hospitali ya Mbarari.
Dkt. Dudange amesema Serikali ya Awamu ya Sita imefanya maboresho makubwa ya miundombinu katika sekta ya afya ikiwemo ujenzi wa Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati.
