Mhadhiri na Padri wa kanisa Katoloki la Roma kutokea Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Mkoani Mwanza, Padri Innocent Sanga ameeleza Sifa ya kipekee ambayo aina yoyote ya kiongozi anastahili Kuipa kipaumbele cha kwanza kwake ni Kumcha Mungu Pekee.
Aidha ameambatanisha na mfano mzuri kuwa Hayati Dkt. John Magufuli alimpenda Mungu hivyo atakumbukwa sana kupitia kile kilichowahi tokea kipindi Uviko 19 ulipotanda nchini kwani hakuacha kusisitiza watu kuchukua taadhari lakini wamche Mungu kwa Imani zao wenyewe.
“Kiongozi mzuri ni yule anayemcha Mungu, Hayati Dkt. John Magufuli alikuwa ni mtu ambaye alimpenda Mungu, tunakumbuka wakati wa Corona imepamba moto alitusisitiza Watanzania kusimama na Mungu” Padri Innocent Sanga, Mhadhiri Chuo Kikuu cha SAUT.