Makamu wa Rais wa Yanga SC, @Arafat__AH ametoa tiketi 1000 za kushuhudia mchezo dhidi ya US Monastir katika mchezo utakaochezwa jumapili ya wiki hii,kwa wote watakaojitokeza kwenye zoezi la uchangiaji damu litakalofanyika siku ya Ijumaa, katika Hospitali ya Mloganzila na Makao Makuu ya klabu ya Yanga.
Ikiwa ni sehemu ya kujali na kusamini utu, klabu hio inafanya hivyo kuhakikisha kunapatikana ongezeko la asilimia nyingi ya damu ili kukizi huduma za matibabu kiujumla pale tu itakapokuwa inahitajika kwa uharaka.