Kiongozi wa Vijana wa Chama Pinzani cha ACT Wazalendo, Abdul Nondo aeleza sababu inayopelekea nchi ya Tanzania inaendelea kukubwa zaidi na changamoto ya Ukosefu wa ajira hasa kwa vijana.
Nondo amefunguka kuwa mfumo wa uchumi usio zalisha ajira ndio chanzo kikubwa kinachopelekea wimbi hili kubwa la ukosekanaji wa ajira hapa nchini.
“Tatizo la ukosefu wa ajira nchini husababishwa na uchumi usio zalisha ajira,mfumo wetu wa Elimu ,Sera mbovu za serikali ya CCM na uwezeshaji usio kidhi kwa vijana.Sisi ACT wazalendo tuna jibu wapi pakutengeneza ajira hasa kupitia kilimo,sekta rasmi na isiyo rasmi” @abdulnondo2