Droo iliyochezeshwa siku ya leo Machi 15,2023 imeifanya klabu ya Yanga iweze kukutana na na kikosi cha Geita Gold kwa mara nyingine tena katika hatua ya robo fainali kusaka ushindi wa kutwaa ubingwa wa kombe la shirikisho la AZAM SPORTS.
Kwa tukio hilo ikumbukwe kuwa siku chache hapo nyuma vikosi hivi vya timu mbili vilikutana na kucheza kandanda safi lililojaa ushindani mkubwa, ambapo klabu ya Yanga iliwiwa vigumu kupata nafasi ya kufunga katika sehemu ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Ila baada ya mchezo kukamilika Yanga ikaibuka kifua mbele kwa ushindi wa jumla ya Goli 3-0 dhidi ya Geita Gold, mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara raundi ya 25 uliochezwa katika Dimba la Chamanzi Complex.