Mkuu wa Idara ya kinywa na meno katika hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando Dokta Emmanuel Motega ameishauri jamii kujiepusha na mambo ambayo ni kinyume na utamaduni wa kitanzania ikiwemo kufanya ngono ya mdomo ili kuepuka vinywa vyao kupata maambukizi ya virusi hatari.
Ushauri huo umetolewa baada na kuwepo watanzania wengi siku za karibuni kuiga mifumo ya maisha ya watu wa jamii ya magaribi hadi kufikia kutumia sehemu ya kinywa kama sehemu inayohusishwa kufanya ngono ambayo baadae inaweza kuleta madhara makubwa katika mfumo mzima wa kinywa na meno.