Watu wa usalama walipojaribu kumpatia mwamvuli wa kumkinga na mvua kali alipokuwa akikagua gwaride la heshima na kupiga saluti, alikataa kuutumia kwa kuwa askari waliokuwa kwenye gwaride hawakuwa na miavuli wenyewe.
Alisikika akisema “Askari waliosimama kwenye mvua pia ni binadamu kama mimi, kulowekwa na mvua hakujawahi kuua mtu. Tunapaswa kukabiliana na yaliyo mbele yetu bila woga wala upendeleo.”